habari Mpya


Ufafanuzi wa Serikali Kuhusu Umiliki wa Laini za Simu Zaidi ya Moja.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye akijibu swali Bungeni mjini Dodoma April 23, 2019.


Serikali imesema haijatoa tamko la kupiga marufuku kumiliki laini nyingi za simu badala yake imelenga kuzuia Mwananchi mmoja kutumia laini zaidi ya moja, kwa mtandao mmoja.Naibu Waziri Nditiye ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ambaye alihoji kuhusiana na kauli hiyo iliyotolewa na serikali hivi karibuni.Mbunge Selasini amehoji kuwa, "Waziri amesema Mei 1, utaanza usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, akasema hakuna kumiliki laini 2 mpaka uruhusiwe, haudhani mtawatesa wananchi kwa maeneo ambayo mitandao mingine haipatikani?".

Akijibu swali hilo ndani ya Bunge Naibu Waziri amesema kuwa, "nilichosema ninatamani kila mtanzania awe na laini moja kwaa kila mtandao, akitaka laini nyingine aseme tu, tunaepuka utitiri wa laini nyingi, mfano ' Zile laini za tuma kwa namba hii ni laini zisizo na tija'".

BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA MAJIBU YA NAIBU WAZIRI.

Post a Comment

0 Comments