habari Mpya


Serikali Yaleta Mabehewa na Vichwa vya treni ya Umeme 1,400.

Muonekano wa uungwaji wa reli ya treni za Umeme, Standard Gauge Railway kuunganishwa kwa vipande vya SGR na kufanya reli hiyo kuwa moja kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam uliofanyika Aprili 14, 2019 katika kijiji cha Soga mkoani Pwani na kuhudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe.
MsemajiI wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Serikali inatarajia kuleta mabehewa na vichwa vya treni ya umeme 1,400.

Waziri Kamwele alieleza kuwa ifikapo mwezi wa saba mwaka huu 2019, Mkandarasi wa reli hiyo ya Shirika la Reli nchini (TRC) wataleta kichwa cha treni ya umeme kwa ajili ya majaribio kwenye kipande cha reli cha Kilometa 30.

Mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea. Reli hiyo itaanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu wa Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda Burundi na DR Congo.

Post a Comment

0 Comments