habari Mpya


Tamko la Rais Dkt Magufuli Kuhusu Usajili wa Laini za Simu Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA) kutowabughudhi watu ambao hawatasajili laini kwa mfumo wa Vidole, katika zoezi ambalo limepanga kuanza Mei Mosi mwaka huu,2019.

Rais Magufuli amesema zoezi hilo haliwezi kufanyika kama ilivyopangwa na TCRA, kwa kuwa sio watu wote wanaomiliki simu wenye Vitambulisho vya Taifa.

Badala yake amezitaka Mamlaka zinazohusika kuendelea na Usajili wa laini kwa watu wenye Vitambulisho tu, huku NIDA wakiendelea kusajili Wananchi ili kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.


MSIKILIZE ZAIDI HAPA CHINI.

Post a Comment

0 Comments