habari Mpya


Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 Wakimbizwa Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma.

Mwege wa uhuru kitaifa 2019 umeanza kutimua vumbi mkoani Kigoma ambapo hapa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Bw.Mzee Mkongea Ally akikagua kitalu cha michikichi katika kata ya Kinazi wilayani Buhigwe.

Na Philmon Golkanus –RK Buhigwe.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Kanali Michael Ngayalina amepokea mwenge wa Uhuru hii jana April 19,2019 ukitokea wilayani Kigoma na ukiwa wilayani humo, umekimbizwa katika kata 8 kati ya kata 20 za Wilaya hiyo ambapo umekagua miradi 8 yenye thamani ya shilingi milioni 852, 161, 151.

Kanali Ngayalina amesema katika miradi hiyo, miradi mitatu imewekewa mawe ya msingi na miradi mitano imezinduliwa Wilaya ya Buhigwe.

Aidha kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Mzee Mkongea Ally amewataka wananchi kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma ili kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments