habari Mpya


Mwenge wa Uhuru 2019 Wahitimisha Mbio Zake Kigoma.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu  Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa Watumishi wa  Idara ya Uhamiaji nchini  hasa wa mikoa iliyopo  mipakani,  kuacha kukiuka taratibu wakati wanapotoa huduma.

Mkongea ametoa wito huo wilayani kakonko mkoani Kigoma wakati akizungumza na wakazi wa wilaya hiyo mara baada ya kukagua jengo la soko la ujirani mwema linalojengwa katika kata ya Muhange.

Amesema kuwa kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya Watumishi wa Idara ya Uhamiaji nchini kufanya udanganyifu katika utoaji wa vibali kwa wageni wanaoingia nchini, japo ambalo.

Mwenge wa Uhuru 2019 umekamilisha mbio zake mkoani Kigoma kwa kukimbizwa katika wilaya hiyo ya Kakonko, ambapo ukiwa wilayani humo miradi yote Sita iliyopitiwa na mbio hizo imekubaliwa.

Post a Comment

0 Comments