habari Mpya


Askari Polisi Ajiua Kwa Risasi Kahama ..Chanzo Ni Kutozaa.

Na Faraja Marco -RK Kahama 97.3.

Askari Polisi wa kituo cha Polisi wilaya ya Kahama H1363 PC Gideon Clement (30) mkazi wa Muleba mkoani Kagera, amejiua kwa kujipiga risasi shingoni wakati akiwa kwenye lindo katika benki ya Access mjini Kahama. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP RICHARD ABWAO amesema tukio la kujiua kwa Askari huyo limetokea Alhamis Aprili 4,2019 majira ya saa moja na nusu asubuhi akiwa eneo la kazi.

Kamanda ABWAO amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto licha ya kuishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na wamekuta ujumbe kwenye simu aliokuwa akiwasiliana na mke wake kabla ya kutekeleza tukio hilo.

…….

Aidha taratibu mbalimbali zinaendelea ili kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda kijijini kwao Muleba kwa ajili ya mazishi huku akiwasihi watumishi wa idara mbalimbali kuepuka kujichukulia maamuzi wenyewe pindi wanapokumbwa na matatizo.

Post a Comment

0 Comments