Na George Binagi- BMG.
Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (pichani) amewataka Wakuu wa Mikoa nchini
hususani yenye madini, kuhakikisha wanasimamia uanzishwaji wa masoko ya madini
kabla ya Juni 31, 2019.
Majaliwa
alitoa agizo hilo March 17,2019 wakati akifungua Soko Kuu la Madini mkoani Geita ikiwa
ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Januari 22,
2019 wakati akizungumza na wadau wa madini kwamba mikoa yote nchini ianzishe masoko
ya madini.
Aidha
Majaliwa ameagiza viongozi wa Serikali kushirikiana vyema ikiwemo kutoa elimu
kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ili kutambua umuhimu wa masoko ya
dhahabu na kuyatumia huku wakihakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa muda
wote kwenye masoko hayo.
Katibu Mkuu
Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema masoko hayo yatasaidia kuinua
soko la madini hapa nchini ambapo kwa Mkoa Geita tayari wizara hiyo imetoa
leseni 18 kwa mawakala wa kununua madini pamoja na leseni 113 kwa madalali.
Naye Mkuu wa
Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema huu ni wakati wa kuendelea kuijenga
Geita mpya kupitia mapato ya ndani yanayotokana na fedha za mgodi na kwamba
Serikali ya Mkoa huo haiko tayari kumvumilia yeyote atakayekwamisha juhudi hizo
huku Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo mkoani Geita, Christopher Kadio akiwasihi
wachimbaji wadogo kutumia Soko Kuu la Madini mkoani Geita kuuza dhahabu zao.
Mkoa wa
Geita umekuwa wa kwanza nchini kuanzisha masoko ya madini ambapo kutakuwa na masoko/
vituo madogo manane ambayo ni Lwamgasa, Nyarugusu, Katoro, Bwanga, Chato Mjini,
Ushirombo, Masumbwe na Msalala huku soko kuu la madini likiwa Mjini Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Soko Kuu la Madini mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa salamu za wizara yake kabla ya
kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wananchi kwenye
ufunguzi wa Soko Kuu la Madini mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya
wizara hiyo kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini nchini.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akitoa salamu za mkoa huo kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa salamu kwa
niaba ya umoja wa mabenki wadau wa uanzishwaji masoko ya madini nchini
ambayo ni NMB, Azania na CRDB.
Banda la Tume ya Madini kutoka Wizara ya Madini.
0 Comments