habari Mpya


Watatu Wafa Mapambano na Polisi Kigoma.

Vitu mbalimbali vinavyosadikiwa kuibwa na kukamatwa na Jeshi la Polisi Kigoma.

 Na Adrian Eustace –RK Kigoma.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limewaua watu watatu  kati ya watano wanaotuhumiwa kuwa majambazi katika majibizano ya risasi baada ya kutekeleza tukio la uporaji wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.3 .
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kigoma.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Martin Ottieno amesema tukio hilo limetokea March 10, 2019 katika kijiji cha Nyarulanga wilayani Kibondo ambapo majambazi hao waliofanikiwa kuliteka gari lenye namba za usajiri T.893 DKY mali ya shirika la GOOD NEIGHBOUR linalohudumia wakimbizi mkoani humo. 

Kamanda Ottieno amesema majambazi hao baada ya kutekeleza tukio hilo walikimbilia katika hifadhi ya pori la Moyowosi wilayani Kibondo. 
Kamanda ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani humo kutoa taarifa za matukio ya kiuhalifu kwa ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

 Nao baadhi ya wananchi mkoani Kigoma wamelitaka Jeshi hilo la Polisi kufanya msako mara kwa mara na kwamba matukio ya utekaji katika baadhi ya mapori mkoani humo yamekithiri na kupoteza amani iliyopo kwa wakazi wa mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments