habari Mpya


Wakuu wa Idara Kakonko Wanaokaa Ofisini Kukiona cha Moto.

Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza na mmoja wa Wananchi katika Vijiji vya Kata ya Nyabibuye alipotembelea..Picha na Maktaba yetu.

Na Amos John –RK Kakonko.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua za kisheria Viongozi wa Idara mbalimbali katika wilaya hiyo wanao kaa ofisini badala ya kwenda kusikiliza kero za Wananchi.

Kanali Ndagala amesema hayo baada ya kupata taarifa za baadhi ya Viongozi wanashinda Ofisini bila kwenda Vijijini kusikiliza kero za Wananchi na hivyo kuchangia kukwama kwa shughuli za kimaendeleo.

Amesema kuwa iwapo ataenda Vijijini kusikiliza kero za Wananchi na kakuta Mkuu wa Idara husika haja chukua hatua za kusuluhisha mgogoro huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

MSIKILIZE HAPA KANALI NDAGALA

Nao baadhi ya Viongozi wakiwemo Wakuu wa Idara wilayani humo wamempongeza Mkuu wa wilaya na kuongeza kuwa kauli hiyo wataitumia kama chachu katika utekelezaji wa majukum yao.

Post a Comment

0 Comments