habari Mpya


Wakimbizi 13 na Watanzania Watatu Wakamatwa na Polisi Kambini Nyarugusu.

Muonekano wa Magunia 700 ya Njegere, 19 ya Unga wa Mahindi yakiwayamekamatwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Kasulu Mkoani Kigoma vikihusishwa na utoroshwaji kutoka katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo wilayani humo.

Picha / Habari na Albert Kavano –RK Kasulu 94.2.
Watuhumiwa.
Watuhumiwa wakiwa na fedha mkononi shilingi milioni 9 wakikamatwa nazo ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal SIMON ANNANGE amesema biashara hiyo inakadiriwa kuingiza zaidi ya shilingi milioni 81 kwa mwezi na kwamba uchunguzi ukikamilika wahusika watafikishwa Mahakamani.

Watuhumiwa 16 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakihusishwa na biashara hiyo, ambao ni wakimbizi 13 na watanzania 3 akiwemo REMIGIUS LAZARO mkazi wa Masumbwe Mkoani Geita ambaye ni  mfanyabiashara na mmiliki wa Magunia hayo.
Magunia hayo yamekamatwa katika Magala yaliyo katika kijiji cha Makere na baadhi ya Nyumba za Wakimbizi Kambini Nyarugusu jambo ambalo limehesabika kuwa ni kosa kisheria.

SIKILIZA HAPA CHINI RIPOTI YA MWANDISHI WETU ALBERT KAVANO –KUTOKA RK KASULU.

Post a Comment

0 Comments