habari Mpya


Wakamatwa na Vitambulisho Feki vya Ujasiriamali Muleba.

Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani Muleba Mkoani Kagera imewakamata watu watatu wa Kata ya Ngenge kwa kosa la kugushi vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo vinavyotolewa na Serikali ya Rais Dkt John Magufuli.
Mhandisi Richard Ruyango.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amesema watu hao walikamatwa March 08 mwaka huu wakiwa wanaprinti vitambulisho hivyo vya vya wajasiriamali wadogo na kisha kuviuza kwa wajasiriamali wadogo kwa shilingi elfu saba hadi elfu kumi. 
Watuhumiwa.

Mhandisi Ruyango amesema kuwa watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa kijiji cha Rwigembe Bw. Fidel Kamugisha, Mmiliki wa mashine za Kuprinti Vitambulisho hivyo Bw. Edson Muganyizi,  na Muuzaji wa Vitambulisho hivyo ambaye pia ni Mgambo wa kijiji hicho Bw. Benson Amon.
Watuhumiwa hao watatu wamefikishwa Mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Post a Comment

0 Comments