habari Mpya


Viongozi Karagwe Malizeni Mgogoro wa Wakulima, Wafugaji Kijiji cha Kanogo.

Na Elen Magambo –RK Karagwe.

Wakulima wa kijiji cha Kanogo Kata ya Nyakabanga wilayani Karagwe Mkoani Kagera wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro wa wakulima na wafugaji unaoendelea katika eneo hilo ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Wakizungumza na Radio Kwizera wamesema kunakila sababu ya serikali ya kijiji hicho kuingilia kati kwakuweka mipaka yakuenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuondoa mgogoro huo.

Wamesema mgogoro huo umedum kwa muda mrefu tangu mwaka 1997 hivyo wanaiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kuutatua haraka iwezekanavyo mgogoro huo ili kudumisha amani na maendeleo katika kijiji hicho.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyakabanga Bw.JUSTINI FIDELIS amewataka wafugaji wenye ng’ombe chini ya 20 kufugia katika kijiji hicho huku akiwataka walio na zaidi ya ng’ombe 20 kupeleka katika maeneo ya Kaundwe na Kashanda yaliyo tengwa na Serikali kwa ajili ya Ufugaji.

DIWANI NYAKABANGA.

Post a Comment

0 Comments