habari Mpya


Tanzania yafuzu AFCON 2019 Kihistoria.

Timu zilizofuzu AFCON 2019 Misiri.

Baada ya miaka 39, hatimaye leo March 24, 2019 Tanzania inafuzu Fainali za Mataifa Afrika AFCON 2019 nchini Misiri kwa kishindo dhidi ya Uganda. 

Taifa Stars imefuzu kama mshindi wa pili wa kundi kwa pointi zake nane, nyuma ya Uganda iliyomaliza na pointi 13 wakizipiku Lesotho iliyomaliza na pointi 6 na Cape Verde pointi 5.  
Taifa Stars imefuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uganda, ambapo Matokeo mengine Lesotho imetoa sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde.

Tanzania na Uganda kufuzu kutoka Kundi L.

Goli la 3 limefungwa kwenye dakika ya 57 AGREY MORIS na kukamilisha idadi ya magoli ya kuongoza hadi sasa ambapo goli la pili limefungwa na ERASTO NYONI kwenye dakika ya 51 na la kwanza limefungwa na SIMON MSUVA kwenye dakika ya 21.

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufuzu AFCON kihistoria, baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na kwa ushindi huu, kila mchezaji atapatiwa donge nono la Sh. Milioni 10, ahadi ya Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, chini ya Mwenyekiti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Post a Comment

0 Comments