habari Mpya


Stori Mbili za Yaliyojiri Siku ya Wanawake Duniani March 8,2019 -Ngara na Kibondo.

Baadhi ya Wanawake wilayani Ngara Mkoani Kagera wakiwa na Mabango mbalimbali yenye Ujumbe wakati wa Maandamano ya pamoja  katika kusherehekea  Siku ya Wanawake Duniani March 8, 2019.

 Katika kusherekea ,Wanawake hao wamegawa zawadi  ya magodoro, sabuni, mafuta, beseni na mashuka zenye zaidi ya shilingi milioni 2 kwa watoto wanaoishi mazingira magumu wa shule za msingi Ngara mjini na Murugwanza ili kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwakuwa nao ni sehemu ya jamii kama walivyo watoto wanaoishi na familia zao vizuri kwani kufanya hivyo kutawafanya waweze kutimiza ndoto zao.

ISIKILIZE HAPA SIMULIZI YA JENEROZ HERMAN-RK NGARA. 

Huko wilayani Kibondo mkoani Kigoma, Wanawake wakishirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali na Ofisi za Maendeleo na Ustawi wa Jamii wamefanikiwa kuwatembelea Wagonjwa waliopo katika hospitali ya wialaya hiyo huku wakiwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni kutambua umuhimu wao katika jamii.

KUTOKA RK KIBONDO MSIKILIZE HAPA SAMUEL MASUNZ.


Post a Comment

0 Comments