habari Mpya


Stori 4 Yaliyojiri Bukoba Kuhusu Lugha Chafu kwa Wagonjwa,Kahama na Maambuziki ya Ukimwi,Ngara Babu aliyebaka Mjukuu wake na Maji Safi Biharamulo.

Baadhi wa Wahudumu wa Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.Picha na Maktaba Yetu.

Kitendo cha baadhi ya Wahudumu wa Afya nchini kuwatolea lugha mbaya Wanawake Wajawazito wakati wa kuwahudumia, imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa Wanawake kujenga tabia ya kutokujifungulia kwenye vituo vya afya huku Serikali nchini ikidai kutokufumbiua macho tabia hiyo.

Kutoka Bukoba Mkoani Kagera Mwanahabari wetu ANORLD KAILEMBO anasimulizi zaidi –MSIKILIZE HAPA CHINI.
- KAILEMBO

Watu 62 wamebaika kuwa na maambukizi ya virusi ya UKIMWI, kati ya watu  zaidi  ya 2000 waliojitokea kupima, kuanzia January mwaka huu (2019) hadi March 14, 2019, kati ya hao  watu zaidi ya 216 walikutwa na tatizo la kifua kikuu, huku  16 wakikutwa na  ugonjwa wa ukoma.

Msikilize Hapa Chini  Mwanahabari SAIMON DIONIZ kutoka Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
- DIONIZ
Kutokana na taarifa iliyotolewa March 14,2019  kupitia kipindi hiki cha Yaliyojiri kuhusu kitendo cha ubakaji dhidi mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kilichofanywa na Babu yake PANKLAS PROTAS Mwenye  miaka 50 wilayani Ngara mkoani Kagera.

Mwanahabari wetu SAMUEL LUCAS amefika Nyumbani kwa Bibi wa Mtoto aliebakwa na Babu yake  ili kujua Undani wa tukio hilo.
- SAMUEL
Maji safi na salama ni sehemu ya haki msingi za Binadamu.

Zaidi ya wakazi  elfu 20, wa Mamlaka ya mji mdogo wa Biharamulo mjini ,wilaya ya Biharamulo mkoani  Kagera  wanatarajia  kunufaika na  huduma ya maji safi na salama  baada ya kukamilika  kwa mradi  mkubwa wa usambazaji wa  maji katika Mamlaka hiyo .

Mwanahabari wetu WILLIAM MPANJU kutoka Wilayani Biharamulo amezungumza na Meneja wa Maji  Bw  SILAJI  ABUDUL ili kujua hali ya utoaji wa  huduma ya maji katika  mamlaka ya mji mdogo  wa Biharamulo.
- MPANJU

Post a Comment

0 Comments