habari Mpya


Rais Kagame Awasili Tanzania kwa Ziara ya Siku mbili ya Kikazi.

Rais wa Rwanda Mheshimiwa PAUL KAGAME akifurahia zawadi ya Kinyago aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI akipokea zawadi ya picha kutoka kwa  Rais wa Rwanda Mhe. PAUL KAGAME mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI akiwa na Rais wa Rwanda Mhe. PAUL KAGAme kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, PAUL KAGAME ameanza ziara ya Siku mbili nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. JOHN  MAGUFULI ambapo wanatarajiwa kutumia fursa hiyo kujadiliana masuala yanayolenga uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo jirani.

Rais KAGAME aliwasili kwenye Viunga vya Ikulu Jijini Dar Es Salaam majira ya saa kumi jioni na kupokelewa na mwenyeji wake Rais MAGUFULI ambaye alikuwa amembatana na Waziri wa Fedha na Mipango pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano.

Akiwa Ikulu Dkt. MAGUFULI akaonesha kumkirimu mgeni wake kwa kumzawadia picha zilizochorwa kwa umahiri wa hali ya juu pamoja na vinyago.

Baada ya zoezi hilo wawili hao wakapata nafasi ya kuketi faragha na kuzungumza kile kilichosababisha kumleta Rais wa KAGAME hapa nchini. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi viongozi hao wanatarajiwa kujikita zaidi kwenye majadiliano ya masuala yanayohusu zaidi mtengamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hii ni ziara ya tatu ya Rais wa Rwanda nchini tangu Rais Dkt. JOHN MAGUFULI aingie madarakani na zinaonekana kurejesha uhusiano imara baina ya nchi hizi mbili jirani na marafiki.

Post a Comment

0 Comments