habari Mpya


Prof.Ndalichako: Wanafunzi wa kike someni kwa bidii mlikomboe taifa

Buhigwe na Albert Kavano habari,
Picha na Adrian Eustace

Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Profesor.Joyce Ndalichako amewataka wasichana nchini Kusoma kwa bidii ili kuongeza ufaulu Katika mitihani yao ya Taifa.

Waziri Ndalichako ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Janda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma alipo tembelea kuona maendeleo ya Shule hiyo na kugundua kuwa ufaulu wa watoto wakike ni Mdogo.
Amesema Serikali inatoa zaidi ya shilingi bilioni 24 kila mwezi kugharamia elimu kwa shule za msingi na Sekondari hivyo hawanabudi kufanya vizuri zaidi kuliko kiwango cha Ufaulu wa sasa ambapo wavulana huwaacha kwa kiwango kikubwa.

Nao Baadhi ya Wanafunzi wamesema kwa kiasi kikubwa wengi hushindwa kufanya vizuri kutokana na Changamoto za uhaba wa walimu,vyumba vya madarasa, maabara na vifaa vya kujifunzia.


Waziri Ndalichako amesema Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni Moja kuboresha na kutatua changamoto za kielimu wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments