habari Mpya


Posi mashine 100 za kukusanyia mapato kutolewa wilayani Kakonko

Kakonko na Amos John
Halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma inatarajia kupokea jumla ya Posi mashine 100 za kukusanyia mapato  kutoka tamisemi na wadau wa maendeleo.

Akizungumza na Radio kwizera mkurugenzi mtendaji wa Halimashauri ya wilaya ya kakonko mkoani humo Bw.Masumbuko Magangilla ameeleza kuwa wanatarajia kupokea mashine 20 kutoka tamisemi na mashine 80 kutoka Bank ya NMB kakonko
Bw.Masumbuko amesema mashine hizo zitawasaidia katika kukusanya mapoto na hivyo kuongeza mapato ya halimashauri ya wilaya ya kakonko
licha ya kutarajia kupokea mashine hizo mkuu wawilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara ametoa  gari moja  kwa kwa ajiri ya kuwasaidia katika ukusanyaji wa mapato ya halimashauli hiyo.

Post a Comment

0 Comments