habari Mpya


Mwalimu washule ya msingi mkoani Kagera Ahukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa

BUKOBA na Anord Kailembo


Mahakama kuu kanda ya Bukoba imemuhukumu mwalimu Respikius Mtazangira adhabu ya kunyongwa hadi kufa,baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Sperius Eradius,aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kibeta iliyoko manispaa ya Bukoba na kumuachia huru mwalimu Herieth Gerard.Hukumu hiyo imesomwa leo Machi 6, 2019 na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Lameck Mlacha.


Katika hukumu iliyosomwa kwa saa mbili,Jaji Mlacha amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ushiriki wa Heriet kwenye kifo cha Sperius, huku Respicius akitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.


Jaji Mlacha amesema Mwalimu Respicius ambaye alikuwa akisimamia nidhamu, alimpiga kwa fimbo ya kawaida mwanafunzi huyo na baadaye kutumia kuni, jambo lililosababisha majeraha kwenye mwili wa mwanafunzi huyo na ni ushahidi tosha kuwa motto alipigwa mara nyingi.


Amesema kuwa Mtazangira alikiuka sheria ya elimu kuhusu adhabu ya viboko, na alitoa adhabu hiyo bila ruhusa ya mwalimu mkuu.


Hata hivyo, Mahakama amemuachia huru Mshtakiwa namba mbili Bi.Herieth Gerard ambaye pia ni mwalimu wa shule ya Msingi Kibeta ikidai kuwa ushahidi uliotolewa juu yake haukuonesha moja kwa moja kuhusika katika kipigo kilichosababisha mauaji ya mtoto huyo


Katika kesi hiyo namba 56/2018, Mahakama imezingatia ushahidi wa daktari wa magonjwa na vifo kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, Dakt.Kahima Jackson ambaye alisema kifo kilisababishwa na mshtuko uliotokana na kipigo.

Post a Comment

0 Comments