habari Mpya


Murusagamba Yapata Milioni 265 Kuongeza Miuondombinu

Serikali imeipatia shilingi milioni 265 Shule ya Sekondari ya Murusagamba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera kwa ajili ya kujenga BWENI, MAKTABA, BWALO NA JIKO, pamoja na VYUMBA VIWILI VYA MADARASA katika shule hiyo, ambayo ina kidato cha kwanza hadi cha sita.

 Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Februari 13, 2019 ofisini kwake; Afisa Elimu Idara ya Sekondari Bw. FIKENI EZEKIEL SENZIGHE na kuitaka KAMATI YA UJENZI, BODI YA SHULE pamoja na WADAU WOTE WA ELIMU washirikiane ili wakamilishe ujenzi huo kwa wakati.

Fedha hizo zimegawanyika katika miuondombinu ifuatayo shilingi milioni 100 zitajenga BWALO, shilingi milioni 75 zitajenga BWENI, shilingi milioni 50 kwa ajili ya kujenga MAKTABA, na shilingi milioni 40 zitatumika kujenga vyumba 02 vya MADARASA.

Bw. SENZIGHE amesema Miradi hiyo itatekelezwa kwa kutumia FALSE AKAUNTI, ambayo inatumika katika ujenzi wa miundombinu ya Serikali katika shule za sekondari na za msingi, huku akisema wamefika shuleni kutoa elimu kwa kamati na Bodi ya shule namna ya kutumia fedha hiyo.

Shule ya sekondari ya Murusagamba ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita; ambapo shule hiyo ina mchepuo wa masomo ya SAYANSI; na wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao ya ndani, kiwilaya, kimkoa na hata kitaifa.

Post a Comment

0 Comments