habari Mpya


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara :Walio vamia eneo la shule ya shule ya sekondari Lukole wajiondoe wenyewe kabla ya serikali kuchukua hatua

Pichani juu ni mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.Aidani John Bahama.
Habari na Simon Dionizi/Picha na Godfrey Bisambi
Mkurugenzi wa halmasauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw.Aidan Bahama amewaagiza wananchi waliovamia eneo la shule ya sekondari Lukole wilayani humo kujiondoa wenyewe kama alivyoagiza waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Williamu Lukuvi

Bw.Bahama amesema hayo muda mfupi baada ya kupokea Risala ya shule katika mahafari ya 9 ya kidato cha 6 kwenye Shule ya sekondari Lukole iliyo somwa na mkuu wa shule hiyo Arone Sekazoya aliyedai kuwa mipaka ya shule hiyo imevamiwa na wananchi
Pichani aliye simama ni mkuu wa shule ya sekondari ya Lukole Aroni Sekazoya.

Amesema serikali haiwezi kumvumilia mwananchi aliyevamia ardhi ya shule nakujenga hivyo hatua zitachukuliwa mapema na atahakikisha anawatuma wataalamu wa ardhi kufika shuleni hapo kwaajili ya kupima mipaka shule
Awali Mkuu wa shule hiyo Bw. Arone Sekazoya amesema wanafunzi walio hitimu kidato cha 6 ni 342 nakwamba wamekuwa wakikabiliwa na changa moto ya kutofanya michezo kutokana na ukosefu wa maeneo ya kuweka viwanja vya michezo
Post a Comment

0 Comments