habari Mpya


Matokeo ya UEFA Champions League March 5 2019, Ajax na Tottenham Zafuzu Robo Fainali.

Real Madrid ikiwa inacheza msimu wake wa kwanza wa UEFA Champions League bila uwepo wa Cristiano Ronaldo wamejikuta wakitolewa katika michuano hiyo na kuvuliwa Ubingwa huo baada ya kutwaa mara tatu mfululizo, kufuatia kipigo cha magoli 4-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu, ushindi wa ugenini wa 2-1 waliowafunga Ajax wiki mbili zilizopita.

Real Madrid sasa wanaondolewa katika michuano hiyo kwa ushindi wa Ajax wa jumla ya magoli 5-3.

Baada ya kutolewa leo katika hatua ya 16 bora ndio wanakuwa wametolewa kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo katika hatua ya mapema zaidi, kwani kwa miaka 9 toka (2010-2011) hawajawahi kutolewa hatua ya 16 bora au robo fainali.

Post a Comment

0 Comments