habari Mpya


Majibu ya Mamlaka ya Maji mjini Kibondo Kuhusu Maji Machafu yenye Matope Bombani.

Na James Jovin –RK Kibondo.
Muonekano wa maji machafu na yenye matope yanayotoka kwenye bomba na picha hii na video zilisambaa zikionesha maji hayo machafu na yenye matope yanayotoka katika mabomba wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

March 9, 2019 Wizara ya Maji ilitoa ufafanuzi kupitia barua iliyoandikwa na kusisitiza kuwa swala hilo linafuatiliwa kwa ukaribu na sio nia ya Serikali kutoa huduma mbovu kwa wananchi.
Hali hiyo imejitokeza wiki iliyopita ambapo baadhi ya Wananchi wa mtaa wa KUMWAI NA KUMWELULO walipiga picha na video wakati maji yakiwa yanatoka na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii, zikionesha maji machafu na yenye tope huku wakiilalamika mamlaka ya maji mjini Kibondo.

March 14, 2019 Mamlaka ya Maji mjini humo imejitokeza na kusema kuwa sio nia yake kutoa huduma ya maji taka kwa Wananchi bali uchakavu wa miundombinu ndio unaopelekea hali hiyo.

Msikilize hapa chini Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Kibondo Bw. FELIX JULIUS akizungumza na Redio Kwizera, amesema kuwa baada ya kusambaa kwa habari hizo idara ya maji ilifanya ukaguzi na kugundua kuwa maji hayo machafu yanasababishwa na uchakavu wa miundombinu

BW. FELIX JULIUS

Post a Comment

0 Comments