habari Mpya

KANAZI SEKONDARY YAPATA MILIONI 25 KWAAJILI YA UJENZIShule ya sekondari ya Kanazi kata ya Kanazi wilayani ngara mkoani Kagera imepokea jumla ya shilingi milioni 25 ili kumalizia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vinavyo jengwa katika shule hiyo kwa nguvu za wananchi
Kauli hiyo imetolewajana na mkuu wa shule hiyo Bw.Elihanani Mshumbusi wakati akizungumza katika mahafali ya kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha kwanza walio chaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari katika shule hiyo

Bw.MATUNDA MLIMA akitumbuiza katika hafla hiyo kwa kupiga zeze
Bw.Mshumbuzi amesema fedha inakuja kwaajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi ambao umeanzishwa ka nguvu za wananchi hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kuendelea kujitolea ilikukamilisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi waanze kutumia vyumba hivyo

Pichani Wanafunzi wa kidato cha Kwanza wakisoma risala kwa mgeni rasmi
Bw.Mshumbuzi amesema fedha inakuja kwaajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi ambao umeanzishwa ka nguvu za wananchi hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kuendelea kujitolea ilikukamilisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi waanze kutumia vyumba hivyo

Aidha ameongeza kuwa fedha hizo zinakamilisha ujenzi huo kuanzi kuezeka majengo hayo hadi samani za ndani ambapo kwa sasa chumba kimoja kimefikia hatua ya linta huku chapili kikiwa hatua ya msingiPost a Comment

0 Comments