habari Mpya


Habari picha.........Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani Wilayani Ngara

PICHA NA GODFREY PHILIPO RADIO KWIZERA
Ni baadhi ya wanawake wilayani Ngara wakiwa kwenye maandamano ya pamoja ambapo wamezunguka kwenye viunga vya mji mdogo wa Ngara wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti katika kusherehekea siku ya wanawake DunianiNi Mbunge viti maalumu mkoa wa Kagera Bi Oliver Semguruka akipokea maandamano katika viunga vya Moorland Hotel


Wanawake (Waandishi) wa Redio Kwizera wakielekea kwenye maandamano wakiwa na bango lao

Ni Bw. Omary Mbwamb, msimamizi mkuu wa vipindi Redio Kwizera akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Redio hii
Ni Bi Auleria Gabriel (kushoto) mwandishi na Muhariri mkuu Radio Kwizera akizungumza katika sherhe hizo ambapo pia ametumbuiza baada ya kutoa wimbo wake unaoitwa ‘Mwanamke’ kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wanawake kupitia wimbo.
Ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele akizungumza na wanawake wa Ngara pamoja na wageni waalikwa
Ni mbunge viti maalumu mkoa wa Kagera Bi. Oliver Semguruka akitoa nasaha zake wakati akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Wilayani Ngara
Ni wanakikundi cha Ngoma kutoka kata ya Nyamiaga wilayani Ngara wakitumbuiza katika maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa wilaya ya Ngara yamefanyika katika viunga vya Moorland Hotel na kuhudhuriwa na zaidi ya wanawake 100

Post a Comment

0 Comments