habari Mpya


Droo ya CAF Champions League Yaipeleka Simba SC Lubumbashi kwa TP Mazembe.

Droo ya CAF Champions League 2018/2019.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC ya Tanzania, itamenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Simba SC ambayo iliwakilishwa na Mwenyekiti, SWEDI NKWABI na Mtendaji Mkuu, CRESCENTIUS MAGORI Katika droo hiyo, itaanzia nyumbani kati ya Aprili 5 na 6,2019 kabla ya kusafiri kwenda Lubumbashi kwa mchezo wa marudiano Aprili 12 au 13,2019.

Katika droo iliyopangwa March 20, 2019 ukumbi wa Aida Ballroom, Marriot Zamalek mjini Cairo, Misri, washindi wa kwanza wa Kundi D, Al Ahly ya Misri watamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, CS Constantine ya Algeria itamenyana na Esperance ya Tunisia huku  Horoya ya Guinea wakicheza na Wydad Casablanca ya Morocco.

Hapa chini ni Droo ya Kombe la CAF Confederation Cup 2018/2019.

Post a Comment

0 Comments