habari Mpya


Chama cha Skauti Tanzania kuunda kamati ya ukuaji wa Skauti wilayani Kahama

Kahama na Faraja Marko
Chama cha Skauti Tanzaniawilayani Kahama mkoani Shinyanga kimedhamiria kuunda kamati maalum ya wazazi itakayo saidia ukuaji wa skauti katika halmashauri zote tatu za wilaya hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Kahama na Kamishina wa Skauti wilaya ya Kahama Bw.Mussa Chama wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa mwanzilishi wa Skauti duniani.

Bw.Mussa amesema kamati hiyo itakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa wazazi ili kuwaruhusu watoto kujiunga na chama cha Skauti kwa lengo la kuwaimarisha kimaadili.
Nao baadhi ya wazazi wenye watoto katika chama cha Skauti wamesema watoto wao wamekuwa wakiimalika kitaaluma, maadili na hata kiafya hivyo wazazi wengine wawaruhusu watoto wao kujiunga na chama hicho kwa malezi 
 

Post a Comment

0 Comments