habari Mpya


Chama cha Biblia Tanzania Chasaidia Watoto wa Mjane EDINA KATOTO -Ngara.

Mratibu wa Msamaria mwema wilayani Ngara Mkoani Kagera, ADAM KAMANA (kushoto)  akimkabidhi  MUTUYEYEZU JEANNE kitanda kati ya  vitanda vinne vilivyotolewa na Chama cha Biblia Tanzania kusaidia watoto wa mjane  EDINA KATOTO anayeishi Mazingira Magumu ambapo watoto wake wane wanalelewa katika kituo  cha Nazareti wilayani Ngara.

Picha na Shaaban Ndyamukama.
Mratibu wa Msamaria Mwema wilayani Ngara ADAMU KAMAna (kushoto) akimkabidhi mjane EDINA KATOTO kiasi cha Sh 400,000 kuanzisha mradi wa ujasirimali na kukabidhi mojwapo ya vitanda kwa ajili ya watoto wake wanaolelewa kituo cha kulea watoto wanaoishi mazingira magumu cha Nazaleti wilayani humo.

Akikabidhi msaada huo March 19, 2019, Mratibu wa Msamaria Mwema wilayani Ngara ADAM KAMANA amesema familia hiyo inamilikiwa na EDINA KATOTO mkazi wa kitongoji cha Nyakafandi kijiji cha Mukubu wilayani Ngara ambaye alifiwa na Mumewe akiwa Mjamzito na katika kujifungua alipata watoto watatu pamoja kwa upasuaji.

Msikilize hapa katika Mahojiano na Mwanahabari wetu SHAABAN NDYAMUKAMA.

-SHAABAN

Post a Comment

0 Comments