habari Mpya


Asilimia 54 ya Watoto wa Kike Kagera Wapewa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Mji wa Bukoba,Kagera.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Asilimia 54 ya watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 mkoani Kagera wamepatiwa chanjo ya kujikinga na maambukizi ya saratani ya Mlango wa kizazi.

Mratibu wa huduma ya mama na mtoto mkoani Kagera Bi. NEEMA KYAMBA amesema hayo wakati akizungumza na Redio Kwizera ambapo amedai kuwa lengo la kutolewa kwa chanjo hiyo ni kuhakikisha ugonjwa huo unabaki historia.

Hata hivyo amesema mwitikio huo watoto sio wa kuridhisha kwani lengo la mkoa ni kumfikia kila mlengwa na kuwaomba wazazi kuwahamasisha watoto wao kujitokeza na kupata chanjo hiyo.

NEEMA KYAMBA

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wa Manispaa ya Bukoba wamesema kuwa ili zoezi hilo liweze kufanikiwa ni lazima liwe shirikishi likiwajumuhisha wazazi na walimu ambao ni walezi wa wanafunzi kwa kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments