habari Mpya


Ajali za Bodaboda Kagera.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za barabarani kutoka vifo 15 kwa kipindi cha mwezi February mwaka jana hadi vifo 8 kwa mwezi Januari na Februari mwaka huu.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera DENIS KUNYANJA amesema hayo wakati akizungumza na redio Kwizera, ambapo ameeleza kwamba ajali zilizotokea kwa kipindi hicho ni 6 na majeruhi ni 7

Amesema kuwa kundi la waendesha pikipiki za abiria ndilo linaloongoza kwa kusababisha ajali ambapo Jeshi hilo limejikita katika utoaji wa elimu, hasa ya utambuzi wa sheria za usalama barabarani.

MSIKILIZE HAPA CHINI RTO DENIS KUNYANJA.


Kwa upande wao baadhi ya waendesha pikipiki za abiria manispaa ya Bukoba wamesema kuwa wanaonekana kuwa wasabishaji wa ajali kutokana na baadhi yao kutokuwa na vigezo vya kuendesha pikipiki ikiwemo kutokuwa na mafunzo.

Post a Comment

0 Comments