habari Mpya


Wananchi Tumieni Mitandao ya Kijamii kujiletea Maendeleo na Siyo Katika Uhalifu.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ATASHASTA NDITIYE ametoa wito kwa wananchi kutumia mitandao ya kijamii kujiletea maendeleo na sio kutumia katika kufanya uhalifu.

Ameyasema hayo leo February 28,2019 wakati akifunga mkutano wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika AFRALT na kueleza kwamba serikali imejipanga vema kwa kuwa na vifaa vya kuwabaini wote wanaotumia mitandao kufanya uhalifu.

WAZIRI ATASHASTA NDITIYE.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilino nchini (TCRA) ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyeki wa Baraza hilo Mhandisi JAMES KILABA amesema uwepo wa chuo cha AFRALT kinachotoa mafunzo ya mawasiliano ni fursa kwa watanzania kujiunga ili kuongeza weledi katika masuala ya mawasilinao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo WILLIAM BARAZA amesema kuteuliwa kwa nchi ya Tanzania kuwa mwenyekiti wa baraza, kutaongeza chachu ya nchi wanachama kujifunza kutokana na uwepo wa maendeleo ya sekta ya mawasiliano nchini.

Mkutano huo wa Baraza la Mawasilino ya Taasisi ya Mafunzo ya Mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, umehitimishwa leo Alhamisi February 28,2019  jijini Mwanza ambapo nchi ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Post a Comment

0 Comments