habari Mpya


Wanafunzi Geita Walilia Maabara Zikamilishwe

                        Geita na Gibson Mika.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Rutozo Mkoani Geita wameiomba serikali na wazazi wao kumalizia ujenzi wa jengo la maabara ili kukabiliana na changamoto ya wao kushindwa kujifunza kwa vitendo.

Wakizungumza mbele ya Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Rutozo, katika ziara ya siku moja ya Jumuiya hiyo ya Kutembela Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuhamasishwa swala la utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa50,Jengo la maabara na walimu wa masomo ya sayansi hali inayowafanya kushindwa kujifunza kwa vitendo.
Hata hivyo,Mkuu wa shule hiyo Bw, Revocatus Maraha amesema uhitaji wa vyumba vya  madarasa ni ni mkubwa  na kwamba vyumba vilivyopo 10 pekee  hivyo wanafunzi hushindwa kujifunza kwa vitendo kutokana na jengo la  maabala kushindwa kukamilika.


Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Rutozo Bw, Shija Baluhya amewataka wanafunzi hao kuwa wavumilivu huku serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili na kuahidi kuwapatia mipira kwa ajiri ya michezo na vitabu 50 vya masomo ya sayansi kwa ajiri ya kuongeza ufaulu wao.
Katika hatua nyingine Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wanafunzi hao wamepanda miti 133 kwa lengo la kutunzaji wa mazingira na kupata  kivuli wanafunzi wakati wa mapumziko.

Post a Comment

0 Comments