habari Mpya


Wabunge watoka mbio ndani ya ukumbi wamikutano ya baada yakulia kengele ya tahadhari


Taharuki imeibuka Bungeni hii leo na kikao kulazimika kuvunjika kwa muda huku wabunge wakilazimika kukimbia kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Februari 5, 2019  asububi baada ya alamu ya Bunge kulia ikiashiria kuwepo kwa tatizo.

 Alamu hiyo imelia wakati Naibu Waziri wa Kilimo,Omary Mgumba alipokuwa akijibu maswali bungeni hali iliyomfanya kukatisha majibu yake kuungana na wabunge wenzake kukimbia kutoka nje.

Alamu hiyo ya tahadhari  ilianza kupiga saa 5:02 hadi saa 5:08 asubuhi na kuanza kulia tena baada ya dakika kama 10.

Hata hivyo mpaka sasa bado chanzo cha alam hiyo kulia bado hakikajulikana

Post a Comment

0 Comments