habari Mpya


Shule ya sekondari Mugoma wilayani Ngara yapata vifaa vya milioni 5

Ngara na Godwin Bruchard
Madawati62 na meza vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5 vimekabidhiwa katika shule ya secondary Mugoma kata ya Mugoma Wilayani Ngara Mkoani Kagera.
 

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya ziwa Abraham Augustino amekabidhi Madwati hayo kwa mkuu wa Wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael Mangwela Mtenjele shuleni hapo.

Akikabidhi msaada huo Bw.Augustino amesema kuwa benki hiyo imejiwekea utaratibu wa kusaidia maswala ya kijamii katika Nyanja ya afya na elim ambapo imetenga jumla ya shilingi bilioni  moja  kwa mwaka huu 2019
Akipokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mangwela Mtenjele amewatakawanafunzishuleni hasa wakike kusoma kwa bidii nakujiepusha mazingira yanayo weza kuwasababishia ujauzito  na kutofikia ndoto zao.

Post a Comment

0 Comments