habari Mpya


Robo Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) Kuchezwa March 2019.

Azam FC imekamilisha timu 8 zinazoenda hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mechi ya jana February 25,2019 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam. 

Ushindi huo  umetokana na mabao ya Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu dakika ya 21, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 54 na Obrey Chirwa dakika ya 69.
Azam FC inakwenda Robo Fainali ikiungana na vigogo, Yanga SC walioifunga Namungo FC  bao 1-0 bao pekee la mshambuliaji wake Mkongo, Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 82 February 24,2019  Uwanja wa Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Timu nyingine zilizotinga robo fainali ni 

Singida United
KMC
Kagera Sugar
African Lyon
Alliance FC
na Lipuli FC 

Michezo ya robo fainali itachezwa March 27-31,2019.

Post a Comment

0 Comments