habari Mpya


Picha Ujenzi Soko la Dhahabu Geita waendelea, wagharimu Bilioni 2.

Muonekano wa Mafundi wa Soko kuu la Geita wakiendelea na Ujenzi wa Ofisi za Soko la Dhahabu ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2.

 Wakazi wa Mjini Geita wanasema kukamilika kwa soko hilo la madini ya dhahabu litawanufaisha WAJASIRIAMALI na WAFANYABIASHARA hususani wamiliki wa nyumba za kulala wageni, Migahawa na hoteli kutokana na ongezeko la wateja wa madini hayo.
Soko hilo linatarajia kuanza mapema MWEZI MARCH,2019 mara tu baada ya kukamili kwa ujenzi wa OFISI ZA TAASISI ZA KIFEDHA, MADINI NA WAFANYABIASHARA WA DHAHABU zitakazokuwa kwenye soko hilo, ambapo Serikali imesema imeamua kuweka ofisi zote sehemu moja ili kumrahisishia mnunuzi wa dhahabu kukamilisha manunuzi yake kwa wakati na pia usalama wa fedha na madini atayonunua.
 
Katibu wa Kamati ya Uanzishwaji wa Masoko ya Madini Mkoani Geita RAMADHAN MCHARO amesema masoko zaidi ya nane yanatarajia kuanza katika Wilaya tano za mkoa huo na kwamba tayari wafanyabiashara wamejitokeza ambapo kuna leseni 13 za DEALERS LICENCE au BROKERS LICENCE, huku ofisi ya madini wakiwa wametoa leseni zingine 114. 
 

Post a Comment

0 Comments