habari Mpya


Nyang'hwale - Makisio ya Bajeti ya Fedha 2019/2020 Yapungua.

Madiwani wa Nyang'hwale wakiwa katika vikao vya kupitia ajenda mbalimbali.

Katika Makisio na Matumizi ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita yameonekana kupungua  kutoka bilioni 1.4 hadi milioni 832.19 ambayo ni sawa na  asilimia 40.6.

Kushuka kwa makadirio hayo ni kutokana na kupungua kwa mapato katika chanzo kikubwa kilichokuwa kikitegemewa na Halmashauri hiyo ambacho ni kodi ya huduma kutoka mgodi wa Bulyanhulu uliopo chini ya Kampuni ya Accaci ambayo uzalishaji wake unadaiwa kupungua kwa asilimia 90.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu ya mpango  na bajeti ya halmashauri kwa mwaka ujao wa fedha 2019/2020 katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani Afisa Mipango amesema mbali na chanzo hicho pia zao la pamba makisio yake yamepungua kutoka milioni 406 kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 hadi kufikia  milioni 125.

Kutokana na kushuka kwa nyanzo vya ndani vya mapato halmashauri hiyo imebuni vyanzo vipya ambavyo vitaanza kukusanya mwaka ujao wa fedha vikiwemo ushuru wa minara, ushuru wa madini ya ujenzi na chanjo ya mifugo.

Post a Comment

0 Comments