habari Mpya


Matukio ya Polisi Wasio Vaa Sare za Kazi yamepungua Bukoba.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba 97.7

Wapanda Pikipiki maarufu Bodaboda Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamesema matukio ya kukamatwa na Askari Polisi wasio vaa sare za kazi yamepungua tangu Wazairi wa Mambo ya Ndani ya Nchi KANGI LUGOLA apige marufuku vitendo hivyo.

Wakizungumza na Redio Kwizera wamesema hatua hiyo imesaidia kupunguza uporaji wapikipiki uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watu walio kuwa wakijifanya Askari Polisi na kuwaibia wananchi pikipiki zao.

Wamesema kuwa nidhamu na mahusiano baina ya bodaboda na askari ni makubwa kwani oparesheni wanazifanya kwa utaratibu unaoeleweka ikiwemo kuvaa sare za kazi hivyo wameahidi kutii maelekezo na sheria za usalama barabarani.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi KANGI LUGOLA alipiga marufuku askari kukamata pikipiki akiwa hajavaa sare za kazi.

WASIKILIZE HAPA BODABODA WAKIZUNGUMZA.

Post a Comment

0 Comments