habari Mpya


Makopo na Ndoo yaendelea Kudhibitiwa na Wakala wa Vipimo Kagera.

Na Wiliam Mpanju -RK Biharamulo.

Ofisi ya Wakala wa Vipimo mkoa Kagera imewataka wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanaojihusisha na biashara ya mazao ya nafaka kuacha mara moja kutumia makopo na ndoo kuwapimia wateja wao kwani watakaobainika hatua za kisheraia zitachukuliwa dhidi yao.

Afisa vipimo mkoa wa Kagera Bw. ANITIKE TUMAINI amesema  wafanyabiashara wanapaswa watumie mzani wa mawe ambayo imehakikiwa kisheria na kwamba atakaye endelea kutumia vipimo hivyo atachukuliwa hatua.

MSIKILIZE HAPA Bw. ANITIKE TUMAINI AKIZUNGUMZA.
Wakala hao wa Vipimo mkoa Kagera wamefanya ukaguzi wa vipimo February 27,2019 kwa wafanyabiashara wa nafaka katika eneo la Nyakanazi na Biharamulo mjini.

Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bi. SADA MALUNDE alilolitoa hivi karibuni baada ya kupokea malalamiko ya wakazi wa Biharamulo na Nyakanazi juu ya vipimo hivyo.

Baadhi ya Wafanyabiashara wa nafaka mjini Biharamulo na Nyakanazi wamesema wamekuwa wakitumia vipimo hivyo kutokana na changamaoto ya kukosa gharama ya kununua mizani kwani gharama yake ni zaidi ya shilingi laki moja.

Post a Comment

0 Comments