habari Mpya


Majeruhi 10 wa ajali ya basi la Frester waendele kutibiwa Hospitali teule Biharamulo mkoani Kagera

Biharamulo Shaaban na Ndyamukama.
Majeruhi 10 wa ajali ya basi la Frester wamendelea kulazwa wakipata matibabu katika Hospitali teule ya Biharamulo mkoani Kagera baada ya 32 kuruhusiwa huku watatu wakipata Rufaa hadi hospitali ya Bugando mkoani Mwanza.

Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Biharamulo, Dkt Edgar Zabron amewataja waliopelekwa Bugando kuwa ni Benitha Burchard (22) na Mathilida Yohana (61) ambapo walivunjika mikono upande wa kulia kila mmoja na Gezila Raulian aliumia kiuno 

"Waliobaki wanaendelea kutibiwa hapa baada ya wengi wao kupata fahamu na kuomba kwenda kutibiwa jirani na makazi yao kwa huduma za kawaida tofauti na dawa zinazotolewa kituoni kwetu na waliobaki tunaendelea kuwahudumia" Amesema Dkt Zabron
Amesema hadi jana jioni walikuwepo majeruhi 18 ambao hali  haikuwa nzuri ni wawili waliokatika mikono  walihitaji wataalamu wa mifupa kwani kituo cha biharamulo hawapo  wataalam hao na kwamba majeruhi wote waliobaki waliumia mikono na miguu ya upande wa kulia.

Aidha, Kaimu kamanda wa jeshi la  polisi mkoani Kagera Isack Msengi amesema ajali hiyo ilitokea jumamosi Februari 2,2019 ikilihusisha basi la kampuni ya Fresta lenye namba za usajili T375 DND iliyokuwa ikitokea Bukoba Kwenda jijini Dar es Salaam.

Msengi amesema cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dreva wa gari hilo lililokuwa na abiria 53 Benjamini Magida (43) alishindwa kukata kona iiliyoko kijiji cha Kasuno kata ya Katahoka wilayani Biharamulo majira ya saa 3:10 asubuhi hatimaye basi kupinduka.


Post a Comment

0 Comments