habari Mpya


Maagizo ya RC Kagera Kuhusu Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima Karagwe.

Mkuu wa Mkoa GAGUTI amemwagiza na kumpa wiki moja  Mkuu wa Wilaya ya Karagwe GODFREY MHELUKA kuanzia leo tarehe 27/02/2019  kufanya uhakiki na utambuzi wa wafugaji wadogo ambao walisajiliwa katika Kijiji hicho cha Kahundwe na kuwaondoa wavamizi ambao ni wakulima na wafugaji wakubwa waliotoka maeneo mengine.

 Pili Mkuu wa Wilaya ya Karagwe GODFREY MHELUKA na timu yake wafanye uhakiki wa mifugo ili kubaini wafugaji ambao kwanza si raia wa Tanzania na pili kubaini wingi wa mifugo kusudi kama kuna wafugaji wakubwa wenye mifugo mingi waondolewe ili wafuate sheria za kuomba vitalu vya kufugia kama wafugaji wakubwa au wawekezaji katika vitalu.

Mgogoro wa wakulima na wafugaji umedumu kwa zaidi ya miaka kumi na moja katika Kijiji cha Kahundwe kata Chanika Tarafa Kituntu Wilayani Karagwe  kulisababisha uvunjifu wa amani uliowahi kutokana na mgogoro huo mwaka 2008.

Post a Comment

0 Comments