habari Mpya


Kesi ya Mauaji ya Mwanafunzi Spelius Eradius Kusikilizwa Kwa Mara ya Pili Leo February 8 Bukoba.

Mkoa wa Kagera katika kuadhimisha kilele cha wiki ya Sheria Februari 6, 2019 Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Bukoba chini ya Jaji Mfawidhi LAMECK M. MLACHA imeweza kusikiliza kwa mara ya kwanza kesi Namba 56 ya mwaka 2018 ya Mwalimu RESPIKIUS PATRICK MTAZANGIRA na Mwalimu ERIETH GERALD dhidi ya mauaji ya Mwanafunzi marehemu SPELIUS ERADIUS wa Kibeta Shule ya Msingi Manispaa ya Bukoba aliyepigwa hadi kupelekea mauti ya kifo chake tarehe 27.08.2018.


Katika shauri hilo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Msomi CHEMA MASWI ,Kaimu Mwendesha Mashitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo aliwasilisha mashahidi saba kutoa ushahidi katika shauri hilo.
WATUHUMIWA .

Shahidi wa kwanza Bw. BENIUS BENEZETH ambaye ni dereva bodaboda aliyembeba Mwalimu ERIETH GERALD siku ya tukio alitoa ushahidi mbele ya Mahakama jinsi alivyombeba mwalimu huyo na kumfikisha shuleni Kibeta na kupokelewa mizigo na wanafunzi.

Baada ya kutoa ushahidi mbele ya Mahakama shahidi wa kwanza Bw. BENIUS BENEZETH na kuhojiwa na pande zote mbili upande wa Jamhuri na upande wa utetezi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba LAMECK M. MLACHA alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 8.02.2019 ambapo mashahidi wengine sita wataendelea kutoa ushahidi wao mbele ya Mahakama.
Kesi hiyo namba 56 ya mwaka 2018 ilisikilizwa mara baada ya hafla fupi ya ufunguzi wa mwaka mpya wa shuguli za Mahakama kumalizika katika viwanja vya Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Bukoba ambapo wananchi na wageni waalikwa waliruhusiwa kuhudhuria na kusikiliza kikao hicho cha Mahakama Kuu kilichoashiria kuwa sasa shughuli za Mahakama Mkoani Kagera zimefunguliwa rasmi.

Post a Comment

0 Comments