habari Mpya


Kanali SIMON ANANGE -Ukosefu wa Elimu ya Sheria Kikwazo kwa Wananchi Kasulu kupata haki.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali SIMON ANANGE amezindua rasimi wiki ya Sheria January 31,2019 katika eneo la Stand mpya Mjini Kasulu huku akiwataka Wanasheria kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi katika wiki hii ya Sheria ili waweze kuelewa Misingi ya kupata haki zao.


Picha/Habari Na Philmon Golkanus-RK Kasulu 94.2.
Mkuu wa wilaya hiyo ya Kasulu amesema ,''-Mahakimu wakitoa hukumu kulingana na vielelezo na ushahidi uliopatikana mbele ya Mahakama hivyo Wananchi hupoteza haki zao kwa kigezo cha kutoelewa namna nzuri ya kuandaa mashauri''.

MSIKILIZE HAPA CHINI. 
Nao  baadhi ya Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakizungumza na Radio Kwizera, Wamesema watatumia Vyema Maadhimisho hayo kuuliza maswali mbalimbali ili kupata kujifunza na ushauri kwa wataalam wa sheria juu ya mambo mbalimbali Mahakamani.

Post a Comment

0 Comments