habari Mpya


Jeshi la polisi wialayani Muleba latakiwa kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kabla ya masaa 24.

Muleba na Shafuru Yusufu.

Wananchi na wadau wa Sheria Wilayani Muleba Mkoani Kagera wameshauriwa kutoa ushiriukiano ili kuwabaini wanansheria vishoka.


Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango amesema hayo jana katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo katika wilaya ya Muleba maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.
Amesema wapo baadhi ya wanasheria wasio rasmi maarufukama vishoka ambao huwa danganya wananchi kwakuwatoza fedha ili wawasaidie kesi zao.
  Amesema wananchi na wadau wa mahakama kuhakikisha wanawabaini watu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria
Aidha ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kutozidisha masaa 24 pale wanapomkamata mtuhumiwa kuhakikisha wanawapeleka mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa wakati ili apate haki yake nakuongeza kuwa hali hiyo itasaidia kuondoa mianya ya Rushwa.
Mwakilishi chama cha wanasheria wa kujitegemea Tanganyika TLS wilayani Muleba Bw.Remidius Mbekomize wameitaka mahakama ya wilaya hiyo kutoa haki kwa wakati ili kuondoa usumbufu unaojitokeza kwa wananchi.

Kwa upande hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Muleba       Bi.Asha Mwetindwa amesema sababu inayopekelekea baadhi ya Mashauri kutokamilika mapema nikutokana na mashaidi kutofika kwa wakati ikiwemo gharama za kuendesha kesi na ushirikiano mdogo kwa wananchi pale kesi inapokuwa katika hatua ya upelelezi.
Aidha katika kipindi cha wiki ya sheria mahakama ya wilaya ya Muleba imewahudumia wananchi zaidi ya 1500 kwa kuwapatia elimu ya sheria ikiwemo kutembelea zaidi ya kata 7.

Post a Comment

0 Comments