habari Mpya


Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita yapitisha Makadirio ya Bajaeti ya zaidi ya shilingi bilioni 77 kwa mwaka 2019/2020


GEITA NA GIBSON MIKA
Halmashauri ya wilaya ya Geita imepitisha makadirio ya bajeti ya kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 77 na milioni 366 na fedha (CSR) Bilioni tano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza mbele ya  Baraza maalumu lililo kaa kwaajili ya  kujadili mipango na bajeti ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2019/2020, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw.Elisha Lupuga amesema bajeti hiyo itaiwezesha halmashauri kutekeleza mipango yake kupitia makusanyo ya  mapato ya ndani na fedha zinazotolewa na wawekezaji kwa ajili ya maendeleo jamii husika.
Hata hivyo,amewataka madiwani kushirikiana na watendaji wa serikali katika kukusanya mapato ya ndani kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo Migodi iliyo katika kata zao.Naye afisa mipango wa halmashauri hiyo,Solomoni Shati amesema mipango na bajeti hiyo imezingatia viapaumbele vya halmashauri hiyo na kwamba atahakikisha fedha zinatekeleza mipango kama ilivyopendekezwa na kupitishwa.


Post a Comment

0 Comments