habari Mpya


Asasi isiyo ya kiserikali ya Nishike mkono yatoa msaada wa Cherehani mbili kwa vijana wawili

Kasulu na Philmon Golkanus
Asasi isiyo ya kiserikali ya NISHIKE MKONO wilayani kasulu mkoani kigoma, imekabidhi chereheni mbili kwa vijana wawili ambao ni yatima waliomaliza mafunzo ya ufundi wa kushona nguo.

Vijana  hao wamekabidhiwa  chereheni hizo baada ya kuhitimu  mafunzo ya ufundi  mwaka huu na kwamba zitawasaidia kujikwamua kiuchumi  kwani  hawakuwa na mtaji wa kuwawezesha wao kununua vifaa hivyo.
Vijana hao wameishukuru Huduma ya Nishike mkono huku wakieleza historia ya maisha yao baada ya wazazi wao kufariki kuwa wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Asasi ya Nishike Mkono Abel Luhamba amesema asasi hiyo kwa sasa inahudumia watoto yatima 102 katika wilaya ya kasulu huku akiiomba jamii kubadili mtazamo na kuona namna ya kuwasaidia yatima na wajane ambao wengi wao wanaishi katika mazingira magumu.

Post a Comment

0 Comments