habari Mpya


Wanajumuia Katoliki Buhororo Washiriki Ujenzi wa Nyumba kwa Mzee Yustas Biziliko (84).

Wazee wasiojiweza ambao ni mume na mke wenye umri wa miaka zaidi ya 75 Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Na Shaaban Ndyamukama- Rk Ngara 97.9

Jumuia ya Wakristo Kigango cha Buhororo Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara mkoani Kagera imetoa msaada wa kuwajengea nyumba waumini wa kigango hicho wasiojiweza ambao ni Mzee YUSTAS BIZILIKO (84) na Mke wake JOSEPHINA YUSTAS (77) kuweza kuishi mazingira yenye usalama.

Baadhi ya Wanajumuia hiyo  wameeleza kuwa  mchakato uliofanyika ni kuhakikisha wanajenga nyumba mpya ya wazee hao baada ya kufanya ziara ya kichungaji na kubaini kuwa Wazee hao wanataabika kwa kunyeshewa mvua kwenye nyumba yao ya nyasi mithili ya kichuguu.

Mmoja wa wanajumuia hivyo ACHILEUS MUBINGE amesema  waliojitolea kujenga nyumba ni rika zote vijana wazee ,waume na wanawake kwa kila mmoja kufanya awezavyo, baadhi wakichota maji, kuchimba mashimo ya kisimika nguzo, kukandika wengine kuezeka.
Mwenyekiti wa Parokia ya Buhororo Mzee STEVEN RUNZAGA mwenye umri wa miaka 75 amesema maisha ya wazee hao yamekuwa ya adha kwani hawana msaada hata wa chakula na walijaliwa kupata watoto lakini  waliwasahau huku wengine pia wakiwa na uwezo mdogo kiuchumi.

Amesema waumini walikusanya miti, matete na makuti ya migomba huku uongozi wa parokia ukitoa mabati na misumari kisha wanajumuia kuungana kila mmoja kwa nafasi yake wakishirikisha na mafundi wanaoshiriki katika jumuia hiyo kuanzisha ujenzi wa nyumba mpya.

Mzee aliyejengewa nyumba YUSTAS BIZILIKO ameshukuru kwa msaada huo na kueleza kwamba hapa anaeleza maisha yake na sababu za kuishi mazingira hatarishi yeye na mke wake.

Hata hivyo uongozi wa kijiji hauna budi kuingiza wazee hao katika mpango Mfuko wa hifadhi ya jamii (TASAF) wa kusaidia wazee hao kupitia fedha za ruzuku kwa kaya maskini na kuwatolea taarifa idara ya ustawi wa jamii angalau  waongeze siku za kuishi.

Post a Comment

0 Comments