habari Mpya


Ukosefu wa Elimu ya Uvunaji na Uhifadhi chanzo cha Mazao kupotea Kigoma.

Na Adrian Eustace –RK Kigoma 94.2.

Imeelezwa kuwa asilimia 85  ya mazao yanayolimwa mkoani Kigoma yanapotea Kila mwaka kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wakulima juu ya uvunaji na uhifadhi wa mazao hayo.

Afisa Masoko kutoka taasisi ya FAIDA MALI mkoani Kigoma Bw.KINANDA KACHELEMA amesema hayo wakati akitoa ufafanuzi wa mradi wa JOINT PROGRAM unaoendelea mkoani humo kwa lengo la kuwaelimisha wakulima juu ya njia bora za uhifadhi wa mazao baada ya uvunaji.
Amesema kwa takribani misimu mitano iliyopita wakulima mkoani Kigoma wamekuwa wakihifadhi mazao yao kiholela katika maeneo yasiyosalama hali iliyopelekea mazao yao kukosa soko la uhakika ndani na nje ya nchi pamoja na kuhatarisha afya za watumiaji.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima mkoani Kigoma wamesema ukosefu wa elimu ya uhifadhi wa mazao kwa muda mrefu ni chanzo kikubwa cha wengi wao kukata tamaa ya kilimo na kwamba Serikali haina budi kusambaza elimu hiyo kwa wakulima nchini ili iwasaidie kuhifadhi mazao ya kilimo vyema.

Post a Comment

0 Comments