habari Mpya


Tazama Matokeo ya Mtihani wa Taifa Darasa la Nne Novemba 2018.

Katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk, Charles Msonde.
 Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Ijumaa Januari 4, 2019 limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa Darasa la Nne Uliofanyika Novemba 2018. 


Akizungumza mjini Dodoma Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt, Charles Msonde amesema kati ya watahiniwa milioni 1 laki 302 na 461 wa darasa la nne waliofanya mtihani huo sawa na asilimia 95.58, waliofaulu kwa kupata daraja A, B, C, na D ni wanafunzi milioni 1, laki 213 na 132 sawa na asilimia 93.16.


Amesema wanafunzi 89,093 sawa na asilimia 6.84 wamepata alama za daraja E ambalo ni ufaulu usioridhisha huku 151 walishindwa kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na utoro.


Dkt Msonde amesema mwaka 2018 takwimu za matokeo zinaonyesha kuwa ufaulu wa watahiniwa kwa masomo yote uko juu ya wastani.“Ubora wa ufaulu umezidi kuimarika kwa kuwa watahiniwa waliofaulu kwa daraja A, B na C umeongezeka kwa asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Post a Comment

0 Comments