habari Mpya


Stori 3 Yaliyojiri Hali ya Usalama Ngara,Geita na Haki Kisheria mkoani Kigoma.

NGARA,KAGERA-RK 97.9.

Hali ya ulinzi na usalama kwa wilaya ya ngara mkoani Kagera imetajwa kuimarika,  huku viongozi wa wilaya hiyo wamezidi kudumisha umoja na mahusiano kwa  wenzao walioko nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Mwanahabari wetu SHAABAN NDYAMUKA amezungumza na Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mntenjele akitaka kujua Hali ya Usalama katika Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.Bofya Play hapo chini Kusikiliza Mahojiano.
GEITA-RK 90.5

Wakazi wa kijiji cha Igate kata ya Nzera mkoani Geita hulazimika kutumia Jeshi la Jadi (Sungusungu)  kujilinda nyakati za usiku kwa kuhofia  kuvamiwa na  watu wanaosadikiwa kuwa vibaka.

Msikilize hapa chini ukibofya play Kutoka Mkoani Geita Mwanahabari wetu GIBSON MIKA anataarifa zaidi.
KIGOMA UJIJI 94.2

Tume ya haki za binadamu nchini imehitimisha awamu ya kwanza ya mafunzo kuhusu haki za Binadamu na Utawala bora kwa viongozi wa sekretarieti ya mkoa wa Kigoma pamoja na wakuu wa idara mbalimbali za mkoa huo.

Kutoka Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu ADRIAN EUSTACE Msikilize hapa chini kwa Kubofya Play anataarifa zaidi.

Post a Comment

0 Comments